 |
| Mh MIzengo Pinda akihutubia WanaUdom toka Rukwa na Katavi |
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni mbunge wa Mpanda Mashariki aliongea na wanafunzi wa Chuo kikuu cha Dodoma jumamosi ya tarehe 16.06.2012. ikiwa ni katika sherehe ya kuwaaga wenzao waliokuwa wakimaliza masomo yao ya Shahada ya Kwanza katika fani mbalimbali,
Katika hafla hiyo Mh. Mizengo Pinda aliwaasa wasomi kutoka mikoa ya Rukwa na Katavi kuwa na kawaida ya kurudi nyumbanio na kuendeleza mikoa yao badala ya kukimbilia miji mingine na kuiacha mikoa yetu ikiwa nyuma kimaendeleo.
 |
| Waziri Mkuu akielekea kupata chakula akiwa na wageni wengine |
Katika Hafla hiyo ambayo pia ilihudhuriwa na Wabunge karibu wote kutoka Mikoa ya Rukwa na Katavi, Pinda alijibu hoja mbalimbali ambazo zilikuwa zimeibuliwa na wanachuo kama vile suala la ajira, kutumia fursa zilizopo za uwekezaji kwa manufaa ya Mikoa hiyo, sambamba na suala la elimu kwa vijana wa Mikoa hiyo. ambapo alieleza mikakati mbalimbali ambayo ipo katika utekelezaji kwa mfano ujenzi wa barabara ya kiwango cha rami toka Sumbawanga hadi Mpanda na pia ujenzi wa chuo kikuu cha Kilimo mkoani Katavi, sambamba na hayo, pia alitolea ufafanuzi miradi ya umeme wa maji ambayo ipo katika hatua za awali za kutafuta wawekezaji ambao watafanikisha upatikanaji wa umeme wa uhakika na wa bei nafuu na kuondokana na umeme wa Mafuta au ule unaonunuliwa nje ya nchi!
 |
| Mh Prudensiana Kikwembe kaitika hafla na Vijana wa Udom toka Rukwa na Katavi |
Hii imekuwa ni mara ya kwanza kwa waziri mkuu kuongea na wanachuo kutoka Rukwa na imekuwa ni faraja kubwa kwa wasomi hawa kuwa pamoja na Wazee wao bila kujali tofauti za itikadi za kisiasa na nyinginezo.
No comments:
Post a Comment