|
||
|
Sunday, September 9, 2012
KUTOKA TANZANIA DAIMA
Thursday, September 6, 2012
POLISI ALIYEMUUA MWANGOZI AKAMATWA
POLISI ambaye alifyatua bomu kwa karibu na kusababisha kifo cha Mwandishi wa habari wa Channel Ten, Daudi Mwangosi, anatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote, Fikra Pevu limefahamishwa.
Taarifa za kutoka Iringa zimeeleza kwamba kushitakiwa kwa askari huyo, kunafuatia kukamilika kwa uchunguzi wa awali ambao unathibitisha pasi shaka kwamba bomu alilofyatua ndilo lililosababisha kifo cha mwandishi huyo wa habari.
Imethibitishwa kwamba kilichousambaza mwili wa mwandishi huyo ni bomu maalumu linalorushwa kwa kutumia bunduki kwa nia ya kusambaza watu waliokusanyika kwa nia ya kutenda uhalifu na lilirushwa kwa karibu mno kinyume cha masharti na kanuni za matumizi yake.
Bomu hilo hutakiwa kurushwa kutoka umbali wa mita kati ya60 na 80, wakati askari huyo alilirusha kwa karibu mno na akimlenga mwandishi Mwangosi.
Katika tukio hilo, bomu hilo liliusambaratisha mwili wa Mwangosi na kumjeruhi ofisa mmoja wa polisi ambaye anaelezwa kutaka kumsaidia mwandishi huyo ambaye alikua akipigwa na polisi wenzake.
Marehemu Mwangosi aliuawa Jumapili iliyopita katika kijijini cha Nyololo, wilayani Mufindi, mkoani Iringa katika tukio ambalo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) walikuwa wakifungua tawi la chama chao, huku Polisi wakitumia nguvu kubwa kuzuia uzinduzi wa tawi hilo.
Jumuiya Ya Vijana Wa CUF: CUF TUNALAANI MAUAJI YA MWANDISHI WA CHANNEL TEN –...
CUF TUNALAANI MAUAJI YA MWANDISHI WA CHANNEL TEN – IRINGA
| Mwenyekiti Wa Cuf Taifa Prof Ibrahim Lipumba-Wa Pili Kushoto akisoma Tamko,kulia kwake ni Mh Kambaya, kushoto kwake ni Mh Mketo na Mh Chalamila. |
CUF –
Chama cha Wananchi tunalaani mauaji ya mwandishi wa Habari wa Channel Ten kituo
cha Mkoa wa Iringa yaliyofanywa na jeshi la Polisi, ambaye pia alikuwa ni
Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari mkoani humo (IPC) Daud Mwangosi
aliyeuwawa kwa kupigwa na bomu (kama inavyosemekana) katika vurugu za kisiasa
baina ya Jeshi la Polisi na Wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA) juzi Jumapili, Septemba 2, 2012 katika kijiji cha Nyololo, wilayani
Mufindi mkoani Iringa.
Kwa
mujibu wa taarifa zinazotatanisha zilizotolewa na Vyombo vya Habari pamoja na
kunukuu taarifa za jeshi la Polisi, kuwa Mwandishi huyo aliuwawa kwa mlipuko
akiwa mikononi mwa jeshi hilo la Polisi hadi kupelekea hata Askari Polisi waliokuwa
karibu yake kujeruhiwa na mwengine kukimbizwa Hospitali.
Taarifa
hizo zinazotatanisha zinasema kwamba Mwandishi huyo alikimbilia kwa jeshi la
Polisi kama kujisalimisha hadi kufikia kukumbatiana na OCS aliyekuwepo katika
eneo hilo la tukio hili ni kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi la Polisi, lakini
wakati huohuo vyombo hivyo hivyo vya Habari vinaripoti kuwa Marehemu alikwenda kumtetea
mwandishi mwenzake wa vyombo vya IPP Media na Polisi huyo OCS alikuwa akimuhami
marehemu asiendelee kupata kipigo kutoka kwa askari wenzake kwani alikuwa
akimfahamu, ndipo hapo alipopigwa na mlipuko huo na kutawanya matumbo yake nje.
Tukio kama hili la mauaji kwa raia katika vurugu za kisiasa baina ya
wafuasi wa CHADEMA na Jeshi la Polisi si la kwanza, ukiacha lile lililotokea
siku za nyuma kule Arusha lililopelekea watu watatu kuuawa, tukio jengine la
kusikitisha ni lile lililotokea Agosti 27, Jumatatu ya wiki iliyopita mjini
Morogoro ambapo mtu mmoja alietambulika kwa jina la Ali Nzona (Muuza magazeti)
alieuwawa katika vurugu kama hizo, ambapo taarifa zake zinautata wakati ambapo
CHADEMA wakidai ameuwawa kwa
risasi, taarifa ya Jeshi la Polisi inasema ameuwawa kwa kupigwa na kitu kizito
kichwani.
Inasemekana
kuwa chanzo cha vurugu zote hizi za Morogoro na Iringa, ni kwa sababu Chama cha
Demokrasia na Maendeleo kimekaidi amri ya Jeshi la Polisi kutokukusanyika ama
kufanya maandamano katika kipindi hiki cha zoezi la uandikishaji sensa
likiendelea hadi hapo litakapomalizika ambapo awali lilipangwa limemalizike
Septemba 1, na baadae kuongezwa siku hadi Septemba 8, awali katika makubalino
ya CHADEMA na Jeshi la Polisi kabla ya mkutano huo ni kwamba walitakiwa
waendelee na mikutano yao.
Kwa
mtazamo huu CUF – Chama cha Wananchi tunaona wanaopaswa kubeba lawama hili ni
jeshi la Polisi na wala si CHADEMA, kwani kama tulivyoeleza awali ilitosha
kuheshimu makubaliano yaliyokuwa yamefanyika baina yao, hata kama kulitokea
vurugu haikuhitajika kutumika nguvu kubwa kiasi hiki.
CUF
pamoja na kulaani mauaji hayo yanaendelea kutokea lakini pia tunasikitishwa na
kupotea kwa nguvu kazi ya Taifa kwa sababu zinazoweza kuepukika, ili hali kuna
uwezekano mkubwa kama busara zingetumika kwa pande zote zinazohusika mauaji
kama haya yasingetokea, kwani tunaamini katika vurugu kama hizo zilizotokea
hakuna zoezi lolote la sensa lililoendelea kufanyika katika maeneo hayo husika
kwa wakati huo.
Kama
hivyo ndivyo ilivyo hakukuwa na ulazima wowote wakuzuia watu kukusanyika au
kuandamana, kwani wanaokusanyika na kuandamana sio wote, bado kuna watu watakao
bakia katika makazi yao ambao wangetosha kutoa taarifa za ndugu na jamaa zao
ambao hawapo au hata kuhesabiwa kwa siku zingine kwani zoezi bado linaendelea,
na waandikishaji sensa wangeweza kuendelea na majukumu yao bila hofu wala
vitisho juu usalama wa maisha yao kutokana na vurugu, kama ambavyo ilivyotokea.
CUF – Kwa kipindi kirefu tumekuwa
tukilililalamikia jeshi la Polisi kuwa liache kufanya kazi kwa ukada bali
lizingatie maadili yake ya kazi ambayo ni kulinda usalama wa raia na mali zake,
matukio
kama haya ya jeshi la Polisi yalianza ndani ya chama chetu, ambapo itakumbukwa
mauaji ya kimbari yaliyofanywa na jeshi hilo Januari 26 na 27 mwaka 2001 wakati
tulipokuwa tukidai Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Daftari la
Kudumu la Wapiga Kura, Tume Huru ya Uchaguzi na kurudiwa kwa Uchaguzi Mkuu wa
Zanzibar wa mwaka 2000.
CUF Tunamuomba
Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuunda Tume Huru itakayoshirikisha Watetezi wa Haki
za Binadamu, Madaktari, Wakuu Jeshi la Polisi na Upelelezi na Wajumbe wengine
kutoka vyama vya siasa ili kuchunguza mauaji haya yenye taarifa za kutatanisha,
ili kuupata ukweli utakaofanyiwa kazi ya kukomesha mauaji kama haya yasiendelee
kutokea, ambayo tunahisi yataendelea kutokea kama hatua madhubuti
hazikuchukuliwa.
Prof. Ibrahim H. Lipumba
MWENYEKITI
Wednesday, August 15, 2012
IJUE KATIBA: INASEMA NINI KUHUSU KULINDA TAIFA?
Kwa taarifa yako tu, Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ibara ya 18 (3) inasema kwamba:-
"Mtu yeyote hatakuwa na mamlaka ya kusaini Mkataba wa KUKUBALI KUSHINDWA VITA NA KULITOA TAIFA KWA MSHINDI, WALA KURIDHIA KUTAMBUA KITENDO CHA UVAMIZI AU MGAWANYIKO WA JAMHURI YA MUUNGANO AU SEHEMU YOYOTE YA ARDHI YA ENEO LA TAIFA NA BILA KUATHIRI KATIBA HII NA SHERIA ZILIZOWEKWA, hakuna mtu atakayekuwa na haki ya kuwazuia raia wa Jamhuri ya muungano kupigana vita dhidi ya adui yeyote anayeishambulia nchi"
Kwa mantiki hiyo, Kama inabidi kupambana na Malawi basi itakuwa ni mapambano mpaka tone la mwisho,
Kwa kuwa Eneo la Ziwa Nyasa kwa upande wa Tanzania linatambuliwa na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama sehemu ya Jamhuri ya Muungano, hivyo basi, kuridhia Wamalawi kuingia nchini kwa namna yoyote ile ni kuvunja katiba ya nchi,
Kujaribu kuigawanya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa namna yoyote ni Kuvunja katiba ya nchi.
Halafu mwisho, inapofikia hatua Rais anatangaza Vita na adui yoyote anayeishambulia nchi, HURUHUSIWI KUPIGA KAMPENI ZA KUZUIA, AU KUWAZUIA raia wa taifa hili kupigana vita ni Uhaini....unastahili kunyongwa....
I love my Country Tanzania
MUNGU IBARIKI TANZANIA
Sunday, August 5, 2012
"MPANDA NDO HOMIE" IN SUPPORT OF KATAVI YOUTHS
For the first time in the history of Mpanda district and the New Katavi Region, the youths who used to be friends on social networks have decided to make a step from just chatting to serving the society.
This has happened when youths from different kinds of social and educational status decided to put their efforts together and conduct an academic colloquium on 27th June, 2012 that comprised about 400 students from ten secondary schools of Mpanda Urban who came together at The St. Mary's social Hall and discuss several issues concerning their academic success as well social development.
The colloquium aimed at inspiring, motivating and encouraging youngsters in secondary schools to put more efforts in achieving their dreams through academic progress. Several topics were discussed among the students. Topics like; relationships in schools led by Miss Shamila Shaban, Academic performances and progress led by Martin Nyambala, Joseph Kulemba and Frank Banka, Reproductive Health to students led by Miss Felister Mbogo and Gamaliel Raiton, Police Jamii led by the representative from Police force Mr. Ngonyani with the OCS of Mpanda. as well the knowledge about internal tourism led by Mr. Japhari Mkelemi and Idd Fumbo
Frankly speaking, all these presentation were hot and successful as students grasped many important ideas and ways to make their success in life and academics and that never giving up and behaving well are the key milestones to their success.
It is now the time for other groups, people and organizations who are committed to conduct different projects and programs for the aim of serving the local people in Katavi so that they play part in then development of their society.
We would like to send our gratitude to all those who made this colloquium to be successful and outstanding, we appreciate all their contributions whether financial or kind contributions, all what was done could not be successful if there were no help from people like these. They are blessed for serving their society.
Friday, August 3, 2012
MALAWI YAITUNISHIA MISULI TANZANIA
- Yakimbilia mkataba wa Berlin wa kuligawa bara
- Tanzania yataka suluhisho
- Msumbiji nao wataka kipande cha ziwa
Malawi
imekataa kuitikia wito wa Tanzania kutaka isimamishe shughuliza
kutafuta mafuta na gesi ziwa Malawi, wakati suluhu ya mvutano wa mpaka
ikisubiriwa
Mvutano
wa maneno umezuka kati ya nchi hizo mbili baada ya Malawi kuipa leseni
Kampuni ya Uingereza kufanya utafiti katika eneo hilo.
Taarifa zinazohusiana
Maafisa
nchini Tanzania wanasema mvutano huo uliodumu kwa miaka 50 sasa unaweza
kuwa mkubwa iwapo ugunduzi wa mafuta na gesi utatokea kwenye ziwa hilo
linalojulikana kama Ziwa Nyasa nchini Tanzania.
Tanzania inasema inaendelea kufanya mazungumzo na Malawi na iko Tayari kulipeleka suala hilo kwenye vyombo vya upatanishi.
"Hili
ni suala nyeti sana na tungependa litatuliwe kwa maelewano, tutaendelea
na mazungumzo," Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania alisema.
Membe
wiki iliyopita alviambia vyombo vya habari nchini humo kuwa "shughuli
za uchimbaji katika eneo la kaskazini mashariki mwa ziwa hazina budi
kusitishwa kupisha mazungumzo kutatua mzozo huo yafanyike."
Malawi, koloni la zamani la Uingereza, kwa upande wake iliapa kuendelea na chughuli za utafiti wa hewa gesi mkaa (hydrocarbons).
Tanzania,lililotawaliwa
na Ujerumani na baadaye Uingereza, inadai kuwa sehemu ya kilometa za
mraba 29,600 sawa na maili 11,400 za ziwa, wakati Malawi inarejea
makubaliano ya mwaka 1890 yanaonyesha kuwa mpaka kati ya nchi hizo mbili
uko kwenye ufukwe upande wa Tanzania.
Msumbiji pia inadai ina sehemu yake katika ziwa hilo la tatu kwa ukubwa barani Afrika.
Mwezi
Septemba mwaka jana serikali ya marehemu Bingu wa iliipa leseni kampuni
ya Surestream Petroleum, kutafiti mafuta na gesi ziwani.
Mataifa hayo mawili yatafanya mazungumzo juu ya mpaka kaskazini mwa Malawi katika mji wa Mzuzu Agosti 20 mwaka huu.
Monday, July 23, 2012
WAZIRI AJIUZURU
Waziri wa Miundombinu na Usafirishaji wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Mh. Hamad Masoud Hamad (Mbunge wa CUF) amejiuzuru wadhifa wake kutokana na mfululizo wa matukio ya Meli Kuzama, katika kipindi chake akiwa waziri zimezama meli tatu, mbili za abiria na moja ya mizigo,
Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar tayari amepokea barua ya kujiuzuru waziri huyo na kumteua mbunge mwingine pia wa CUF kushika wadhifa huo..
Hongera Mh. Hamad kwa kuonesha mfano katika suala la uwajibikaji.
Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar tayari amepokea barua ya kujiuzuru waziri huyo na kumteua mbunge mwingine pia wa CUF kushika wadhifa huo..
Hongera Mh. Hamad kwa kuonesha mfano katika suala la uwajibikaji.
Subscribe to:
Posts (Atom)
