Friday, July 20, 2012

Ujana na mitoko ya nywele!

Siku zote kila mtu hupenda kufanya jambo ambalo anaamini linamfariji, katika kufanya hivyo watu wamekuwa wakitumia muda mwingi pengine na fedha nyingi ili kuitafuta furaha. wapo wanaotumia fedha nyingi ili kupata chakula kizuri, mavazi mazuri, na vitu vingine vinavyofanana na hivyo ila hili suala la nywele limekuwa likivuta kasi katika kutengeneza maisha ya vijana.


Vijana wengi wamekuwa wakiamua kutoka na muonekano wa tofauti ambao unaweza kufanya kila mtu akajua uwepo wake, pamoja na mavazi ya aina yake lakini hili la nywele limechukua sehemu kubwa ya mitoko ya vijana.
 
Hii hapa ni style ya kunyoa ya jamaa mmoja huko kwa wenzetu, usidhani kuwa katumia sh.5000 za madafu kutokelezeiya kistyle hii, hapa ni gharama imetumika, na kum-maintain mdudu huyo kichwani si kazi ndogo, inakulazimu kila baada ya siku mbili au tatu ufike saloon ili kumrekebisha Saramanda kichani pako.

Hahaaa...hii nayo ni mpya, jamaa kaamua kujenga nyumba kichwani pake, style kama hii kwanza inataka moyo, kwanza suala la kulala sijui linatatuliwa vipi hapa. kimsingi jamaa katokelezeiyaa, ila hapo hata kuinama naamini ni issue kwa kuwa anaogopa nyumba yake itaanguka, au kufumuka, sasa hapo usiniulize T-shirt round colar itavaliwaje, na inawezekana ndo maana jamaa kaamua kuwa kifua wazi ili kuepusha bugdha ya kuvaa na kuvua nguo, style ya nywele kama hii inakulazimu kutojishughulisha na lolote zaidi ya kuzilea nywele zako. 
 
 
 
 
 
 
 
Haya kazi kwenu vijana mnaopenda kutokelezeiyaaa...mitoko mingine ni kujitia gharama zisizo na tija! kitu ambacho wengi watengenezaji wa nywele za style hii wanakumbana nacho ni kushindwa kufika sehemu ambazo zinahitaji maadili ili kuingia na kupata huduma, kwa Tanzania yetu vijana wengi wamekuwa na kawaida ya kuiga mitindo ya nywele ya mastaa mbalimbali wa mchezo hasa mpira wa miguu, mitindo kama ya Ronaldo enzi zile ilivuma na vijana wengi walitumia mitindo hiyo, hivi Karibuni umekuja mtindo wa kunyoa kama Baloteli ambao kwa style ya namna yake hadi wazee nao wameonekana kupenda style hizo na kunyoa! haya kazi kwenu.

No comments:

Post a Comment

Tafisiri