Boti, mali ya shirika la Seagul, inayosemekana kuzama hii leo
Habari zilizotufikia hivi punde ambazo hazijathibitishwa zinasema, Boti moja mali ya Kampuni ya Seagul iliyobeba abiria zaidi ya 200 imezama katika bahari ya Hindi, eneo la Shumbe ikitokea Dar-Es-Salaam kuelekea Zanzibar, hii itakuwa ni ajali nyingine kubwa inayogharimu roho za mamia ya Watu ndani ya kipindi kisichofikia mwaka mmoja, tarehe 10 September meli ya kampuni ya Mv Spice Islander ilizama pia katika bahari ya hindi na kusababisha vifo vya abiria, tutaendelea kutoa updates za ajali hiyo kadiri habari zitakavyotufikia.
Meli ya Mv. Spice Islander ikizama katika bahari ya Hindi tarehe 10.09.2011
No comments:
Post a Comment