Thursday, July 19, 2012

TANGAZO LA KAZI YA MUDA YA SENSA


  
Serikali  ya  Jamhuri  ya  Muungano  wa  Tanzania,  inakamilisha  maandalizi  ya  kufanya  Sensa  ya Watu  na  Makazi  ambayo  itafanyika  tarehe  26  Agosti,  2012.  Ili  kufanikisha  Sensa  hii,  Serikali inatangaza nafasi  za  kazi za muda  za MAKARANI NA  MAKARANI  WAANDAMIZI  WA SENSA kwa Watanzania  wenye  nia  na  sifa  zinazostahili  kama  ilivyoainishwa  katika  tangazo  hili.  Kazi  hii itaanza tarehe 06 Agosti, 2012 na kumalizika tarehe 14 Septemba 2012.

1.    KARANI WA SENSA
Kazi za Kufanya
Mwombaji wa nafasi hii, endapo atachaguliwa atapangwa katika eneo analofanyia kazi au eneo analoishi na atakuwa na kazi zifuatazo:-
a)    Kuhudhuria mafunzo ya kuhesabu watu;
b)    Kuhesabu watu kwa kutumia  dodoso fupi  katika Eneo la Kuhesabia Watu na kuhakikisha
kuwa kila mtu anahesabiwa na anahesabiwa mara moja tu;
c)    Kutunza vifaa vyote na nyaraka za Sensa katika hali ya usafi na usalama; na
d)    Kufanya kazi nyingine zinazohusiana na Sensa atakazopangiwa na Kiongozi wake . 

Sifa za Mwombaji
Mwombaji wa nafasi hii anatakiwa awe na sifa zifuatazo:-
a)    Awe na umri usiozidi miaka 60 na mwenye afya njema;
b)    Awe amehitimu angalau kidato cha nne;
c)    Awe  ni  Mkaguzi  au  Mratibu  wa  Elimu,  Mwalimu  katika  Chuo  cha  Ualimu,  Shule  ya
Sekondari au Shule  ya Msingi (Shule za Serikali au Binafsi) katika eneo husika,       AU
d)    Awe ni mfanyakazi yeyote wa umma anayeishi au kufanya kazi katika eneo husika,       AU 
e)    Kijana aliyehitimu masomo yake na hajapata ajira, na
f)    Asiwe na kesi yoyote ya jinai.

2.    KARANI MWANDAMIZI WA SENSA
Kazi za Kufanya
Mwombaji wa nafasi hii, endapo atachaguliwa atapangwa katika eneo  analofanyia kazi au eneo
analoishi na atakuwa na kazi zifuatazo:-
 
a)    Kuhudhuria mafunzo ya kuhesabu watu,
b)    Kuhesabu  watu  kwa  kutumia      dodoso  refu   katika  Eneo  la  Kuhesabia  Watu  na
kuhakikisha kuwa kila mtu anahesabiwa na anahesabiwa mara moja tu,
c)     Kutunza vifaa vyote na nyaraka za Sensa katika hali ya usafi na usalama, na
d)   Kufanya kazi nyingine zinazohusiana na Sensa atakazopangiwa na Kiongozi wake .


Sifa za Mwombaji
Mwombaji wa nafasi hii anatakiwa awe na sifa zifuatazo:-
a)    Awe na umri usiozidi miaka 60 na mwenye afya njema,
b)    Awe amehitimu angalau kidato cha sita,
c)    Awe  ni  Mkaguzi  au  Mratibu  wa  Elimu,  Mwalimu  katika  Chuo  cha  Ualimu,  Shule  ya
Sekondari au Shule  ya Msingi (Shule za Serikali au Binafsi) katika eneo husika,       AU
d)    Awe ni mfanyakazi yeyote wa umma anayeishi au kufanya kazi katika eneo husika,       AU 
e)    Kijana aliyehitimu masomo yake na hajapata ajira, na
f)    Asiwe na kesi yoyote ya jinai.

3.    Namna ya Kutuma Maombi
Mtanzania  mwenye  sifa  zilizotajwa  hapo  juu  atume  maombi yake  kwa  Mwenyekiti  wa  Kamati ya  Sensa  ya  Wilaya/Halmashauri  kwa  anuani  iliyowekwa  hapa  chini,  akiambatisha  nakala  za vyeti na nyaraka muhimu ili kuonyesha sifa alizonazo. 

Maombi  hayo  yatumwe  kwa  kujaza  Fomu  Maalum  ya  maombi  ya  kazi  ambayo  inapatikana katika  Ofisi  ya  Mratibu  wa  Sensa  wa  Wilaya/Halmashauri,  na  endapo  fomu  haikupatikana, mwombaji atume maombi kwa kuandika barua akionyesha anuani kamili ya mahali anapofanyia
kazi  na namba ya simu kama anayo.

Maombi  yapitishwe  kwa  wakuu  wa  kazi  kwa  walioajiriwa    au  Watendaji  wa  Mtaa/Kijiji    kwa
wale wasiokuwa na ajira, ili maombi hayo yafike    wilayani kabla ya tarehe 25 Julai, 2012.

Mwenyekiti wa Kamati ya Sensa ya Wilaya
Wilaya ya  
S.L.P  


www.nbs.go.tz/index.php?

No comments:

Post a Comment

Tafisiri